Faza wa Burundi: Mchezo wa Shetani Uliowageuka!
Basi bwana, kama kawaida yetu ya kuchota umbea moto moto, leo Cha Umbea TV tumetua nchi jirani — Burundi, na simulizi ya leo inahusu wanandoa walioshikana mikono kwenye njama ya kishetani, lakini mambo yakawageuka mpaka sasa bado hawajapumua!
Habari yenyewe inakwenda hivi...
Kuna mwanandoa mmoja na mkewe, waliamua kuingia kwenye dili la kitapeli. Wakaweka kikao cha ndani wakakubaliana hivi: Mke aende kwa "Faza" – mzee mmoja mwenye hela, mwenye heshima mtaani na mchungaji wa kanisa – kisha acheze karata ya mapenzi. Akishamvutia na kukubaliana kukutana mahali, basi mume aje "afumanie", halafu wamkomoe kwa kumtishia kufichua fedheha hiyo hadharani kama hatoweka hela benki – na si hela ya ugali bwana, walitaka mamilioni!
Kwao walidhani ni mpango wa kisasa, kumbe wameingia kwenye uwanja wa Faza ambaye ni mtaalamu wa michezo ya kichawi na kimagumashi. Jamaa anajua kila kona ya mchezo huu – siyo wa jana mjini!
Sasa mambo yakaanza kama walivyopanga. Mke wa jamaa akapiga simu kwa Faza, akaweka sauti ya mahaba ya kishetani, akapendekeza wakutane hoteli moja ya kifahari. Faza akamkubalia kwa bashasha – akajifanya mtego haujamgusa.
Siku ya tukio ikafika. Mke akavaa mlegezo wa kusadikika, akapulizia perfume ya kutisha, akajitupa hotelini. Hakuwa anajua kuwa Faza alishawasiliana na watu wake wa "chini kwa chini", walikuwa tayari wameshachora network ya kijasusi.
Mke alivyoingia tu mlangoni, kabla hata hajashusha pochi, akapigwa kitambaa cheupe puani chenye dawa kali. Dakika mbili baadaye, hakujuwa ni wapi alipo wala jina lake mwenyewe. Wakamtoa fasta kwa njia zao za kichawi, wakamhamishia hoteli nyingine ambayo hawakujua hata Google!
Sasa huku nyuma, mume yupo moto tayari! Keshapanga kila hatua ya kumfumania mkewe. Akamfuata mhudumu wa hoteli kwa sauti ya kujiamini:
"Bwana, mke wangu yupo chumba fulani na mwanaume mwingine. Nataka nimfumanie na kuweka mambo hadharani!"
Mhudumu akajipatia "kitu kidogo" na kuingia mtego. Akapiga simu kwa mgambo wa hoteli. Wakatayarisha funguo ya akiba – wakafika mlangoni, wakapiga hodi ya heshima – kimya. Wakafungua mlangoni... hamadiiii!
Ndani walikuta watu wengine kabisa – kijana na mpenzi wake, wakitazama runinga kwa raha zao. Yule kijana akafura kama pilipili kichaa, akatishia kuishtaki hoteli kwa kuvunjiwa faragha. Akaanza kufoka, “Hii ni kashfa, ni fedheha, ni aibu isiyoandikika!”
Mume sasa akachanganyikiwa – hajui mke yupo wapi, hajui atoe maelezo gani. Hali hiyo ilimvuruga akili mbaya! Yani ni kama mtu aliyefungua mlango akadhani ni sokwe, kumbe ni simba.
Cha kushangaza zaidi, wiki ya tatu mke hajulikani yuko wapi! Simu yake imezimwa, haonekani mitaani, hata kwao hawamjui alipo. Polisi hajapewa taarifa rasmi kwa sababu mume anaogopa kuaibika – angepiga ripoti atasemaje? "Mke wangu alikwenda kuvuta hela kwa mpango wa kusingizia fumanizi?"
Na sasa Faza yupo zake kanisani kila Jumapili, anakunja suti yake kama kasisi wa Vatican. Anaongoza sala kwa ustaarabu, watu wanampa heshima kubwa, kumbe nyuma ya pazia, wambea wanasema mzee kamuweka mke wa mtu sehemu "anakula tu na kulala", kana kwamba ni “project ya muda mrefu”.
Watu wa mtaa wanabaki kushangaa, "Kumbe hela zinaweza kupumbaza hadi wanandoa kugeuka wezi wa hadhi ya kiroho!" Ila pia, wamegundua kwamba mchezo wa kumtapeli Faza ni sawa na kuchezea nyuki ukiwa umevaa asali.
Cha kusikitisha – mume sasa hivi kabaki kimya kimya, kaamua kugumia machungu. Marafiki wakimuuliza, anacheka kwa huzuni na kusema:
“Maisha haya bwana... si kila dili ni dili!”
USIKOSE episode ijayo ya Cha Umbea TV – sehemu pekee unayojua ukweli usiochapishwa kwenye gazeti. Pale penye moshi, kuna moto wa umbea! 🔥

Post a Comment