Header Ads

test

Boss Kasafiri Lakini Masikio Yapo Ofisini: Chawa Special Unit!


DOMO LA ZAI

Aaah basi bwana leo tumewavaa wale maboss wanaosafiri kikazi au kwenda likizo, lakini hawatoki kabisa kiroho. Yani mwili uko Mtwara kwenye semina, lakini masikio yako pale ofisi ya Kinondoni kwenye jumba la ghorofa la kijivu. Hawa ndo tunawaita "maboss wa CCTV ya roho" – kila taarifa wanaitaka, kila neno wanataka kujua nani kamesema, nani kachelewa, nani kamuamkia nani bila kuinamisha mgongo.

Lakini sasa, boss kama huamini mtu yeyote, ulikuwa unaenda wapi? Umekabidhi ofisi kwa msaidizi, lakini bado kila saa simu:

“Vipi, Mussa kaja kazini?”
“Martha alivaa ile sketi fupi tena?”
“Hamisi bado anakula mihogo ofisini?”
“Leo nani alitoka mapema?”

Yani boss anakuwa amevaa beach short lakini akili ipo kwenye spreadsheet ya attendance. Huku hoteli ya kifahari anainama kwenye simu, anashusha voicenote ndefu kama muhubiri:

“Natambua niko mbali lakini muwe na nidhamu kazini kama nipo, kumbukeni Ofisi sio ya mama yenu!”

Sasa cha ajabu zaidi – hawa maboss hawatendi peke yao! Wanakuwa na mtandao wa kijasusi wa chawa waliowatengeneza maalum kwa upelelezi wa ndani.

Yani mtu anayeitwa "driver" lakini akifika ofisini hana kazi nyingine ila kufuatilia nani anachelewa, nani anaongea vibaya kuhusu boss, nani amekula chakula cha lunch bila kuchangia. Halafu taarifa zinaenda kwa boss kama ripoti ya intelligence:

“Bosi, kuna harufu ya uasi. Watu wanasema ukirudi tu tukutane HR!”
“Bosi, yule mhasibu wako alikuja na mwanamke, walikaa ndani zaidi ya saa moja.”

Wale chawa bwana ni noma. Kazi yao sio productivity, kazi yao ni "reporting kwa hisia na exaggeration". Hawachoki kuchochea!

Ukiwaona kazini, utadhani ni watu wa kawaida lakini wana function kama CCTV ya kishetani. Wanaweka status za boss kwenye profile zao:

“Tuna imani na uongozi wako bosi wetu mtukuka!”

Kumbe mioyoni wanangoja boss atoke watangaze uhuru wa pili wa Tanganyika. Ila bosi akirudi tu, wanabadilika:

“Bosi siku hizi ofisi bila wewe ni kama injili bila Yesu!”

Chawa mwingine huwa anajipendekeza hadi boss anamsaidia hata kusahau kazi zake za msingi. Anaweza kukupotezea promotion yako kwa sentensi moja tu:

“Yule bosi alikuwa anapiga simu wakati wa mkutano. Wengine tuko serious bosi, wengine sijui!”

Wachawi wa kisasa hawa! Wako na boss kwenye roho, si kazini.


Sasa tunajiuliza:

🔹 Boss, kama huwezi kuamini timu yako ukiwa mbali, unawezaje kuwaongoza ukiwa karibu?

🔹 Na wewe chawa, mpaka lini utaishi kwa kumpelelezea watu badala ya kujenga CV yako?


Usikose sehemu ijayo ya Cha Umbea TV, tukiwasha spotlight kwa maboss wa CCTV ya moyo na machawa wao wa FBI ya vibatari. Hawa ndo wanafanya watu wazime kompyuta mapema wasionekane kwa kamera ya roho! 🎥🔥


No comments